2. Utangulizi

Katika makala hii unaweza ukapata machache yatakayokusaidia kufahamu historia ya Parokia hii ya Makambako.

Mojawapo kati ya hatua za maandalizi ya jubilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Parokia ya Makambako, iliyoadhimishwa mwaka 2004, ilikuwa ni kutafuta habari mbalimbali za zamani na kiistoria zihusuzo parokia yetu pamoja na uinjilishaji wa Makambako. Tulimwomba mzee Michael M. Kayombo, mwalimu mstaafu tena kiongozi maarufu katika kanisa la Makambako miaka ya nyuma.

Kwa bidii mzee huyo aliitikia wito huo, akiwahoji wazee mbalimbali wakazi wa Makambako mpaka tukafaulu kupata habari mbalimbali za kiistoria kuhusu Makambako, ambazo tulizikusanya katika kijitabu cha maelezo ya Jubilei.

Kuanzia leo, tutaziweka pia katika tovuti ya parokia yetu katika kipengere hii cha “HISTORIA NA MENGINEYO”

Tunamshukuru Mzee wetu Kayombo kwa kazi kubwa aliyoifanya ili habari nyingine za zamani zinazohusu parokia yetu na mji wetu wa Makambako zisipotee.

Vile vile kama wewe msomaji unazo habari nyingine au ulishuhudia au kusikia kuhusu matukio fulani ya zamani ya parokia yetu, tafadhali utujulishe na sisi – ukitumia anuani ya barua pepe iliyopo kwenye kipengere cha ‘UTAMBULISHO” – ili tuziingize katika tovuti yetu na ziendelee kutajirisha historia yetu.

Vile vile kama unazo picha za zamani za matukio mbalimbali ya kikanisa au picha za mazingira ya Makambako, zinakaribishwa tu.

Tunatoa shukrai kwako pia kwa kutusaidia kukamilisha historia ya Parokia yetu.

Kwa hayo yote unaweka ukatumia pia anuani yetu iliyoandikwa hapo chini:

Mhesh. Paroko

Parokia ya Makambak

S.L.P. 1005

MAKAMBAKO

Nessun commento: