6. La Casa: alcune parole comuni

A. Questa e’ la mia famiglia: noi genitori e due figli.

Hii ni familia yangu: sisi wazazi na waana wawili.

B. Mi hai presentato anche il nonno e la nonna:

Sono venuti a visitarvi?

Umenitambulisha pia babu na bibi:

Wamekuja kuwatembelea?

A. Si. Loro vivono al paese,

vicino alla citta’ di Njombe.

Ndiyo. Wao wanaishi kijijini,

jirani na mji wa Njombe.

B. Grazie. Ora ho capito.

Asante. Sasa nimeelewa.

A. E ora ti mostro la mia casa.

Na sasa nakuonesha nyumba yangu.

B. Vedo che e’ nuova!

Naona kwamba ni mpya!

A. Si, questa costruzione ha solo due anni.

Ndiyo, jengo hili lina miaka miwili tu.

B. Questa stanza e’ la sala.

Chumba hiki ni sebule.

A. Quelle tre stanze sono le camere da letto.

Vyumba vile vitatu ni vyumba vya kulala.

A. Questa e’ la cucina

Hiki ni jiko

A. Questa porta e’ del bagno (WC e doccia)

Mlango huu ni wa choo na bafu.

A. Apri la finestra:

puoi vedere l’ orto con diverse qualita’ di verdura.

Fungua dirisha:

unaweza kuona bustani yenye aina mbalimbali za mboga.

B. Vedo anche molti mattoni.

Naona pia matofali mengi.

A. Sono del mio vicino:

ha in programma di costruire un piccolo negozio.

Ni ya jirani yangu:

ana mpango wa kujenga duka dogo.

Nessun commento: