4. Mazingira ya kiimani kabla ya ujio wa Shirika la Wamisionari wa Consolata

Matokeo ya uchunguzi na mawasiliano ya wazawa halisi wa Makambako inaonesha kuwa eneo hili lilikaliwa na watu wachache sana. Sehemu kubwa ya nchi ilikuwa mapori.

Neno la Mungu kama linavyojulikana leo kwa watu wote halikuwepo. Lakini watu wa zama hizo walikiri kuwepo kwa Mungu aliyefananishwa na upepo. Hivyo walimwenzi kufuatana na mazingira ya wakati huo wa giza. Mungu huyu walimwita kwa jina tukufu “Unguluvi”, yaani Mungu Mkuu.

Historia inaonesha watu hawa walitambua kuwa wao ni wenye maovu siku zote ya kumchukiza huyu Unguluvi, Mungu Mkuu. Hata hivyo waligundua kuwa mababu wao waliokufa ni bado hai na wanaishi pamoja na huyo “Unguluvi”. Kwa mwelekeo huo wa kiroho na mang’amuzi ya kimazingira, wakaamini kuwa ingawa wao hawawezi kusikilizwa na huyo “Unguluvi” kutokana na maovu yao, lakini dua zao na maombolezo yao yakipitia kwa hao mababu zao, huyo Mungu Mkuu atawasikiliza na kuwatendea kile waombacho.

Hivyo ndivyo walivyohusiana na Unguluvi katika nyanja zote za maisha yao mpaka ujio wa Habari Njema ulipowafikia.

Nyakati hizo za giza, maeneo ya mijini na kwenye vituo maalum vya wasafiri, dini ya Kiislamu ilipenya kwa urahisi. Hivyo ndivyo ilivyokuwa hapa Makambako kabla ya madhehebu mengine ya kikristo kuingiza Neno la Mungu.

Bwana Fashel Mlad toka Rujewa akisaidiwa na wana Maburusi wen-gine, aliingiza dini ya Kiislamu. Msikiti mama ungali ukiheshimika na Waislamu wote mpaka hivi leo hapa Makambako na nyumba yake Fashel Mlad kama ukumbusho iko mpaka leo.

Mwitiko wa watu kuingia Uislam kwa wakati huo ulikuwa mdogo sana. Walikuwa waumini wacha-che na familia zilizojitokeza zaidi ni za ukoo wa hayati Rajabu Nganiyavanu na Rajabu Kisingile.

Mzee Mwanzali Gadau akiwa Rugaruga wa eneo lote la Kitisi aliwakataza familia yake kutojihusisha na Uislamu. Alitamka maneno ya busara kama haya, “ Sitaki wanangu kuingia Uislamu, Tusubiri jua”! Alikuwa na maana sana kwa usemi huo. Bila shaka habari za kazi njema zilizokuwa zikifanywa na watawa wa Consolata kule Utengule (Malangali) zilienea mahali pengi zikitoa ujumbe wa kimisionari. Huenda na bila shaka nguvu ya yule aliye juu ilimpa tumaini njema la kuwa na subira ya Jua kujitokeza.

1 commento:

Anonimo ha detto...

i genuinely adore all your posting choice, very interesting.
don't give up as well as keep creating seeing that it just simply very well worth to follow it,
excited to look over way more of your own well written articles, have a good day!